Kinyozi mbaroni kwa kulawiti na kubaka mtoto kwa kumhonga chapati

0
42

Jeshi la polisi mkoani Geita linamshikilia Simon Faida (24) mkazi wa kijiji cha Msasa, kata ya Busanda mkoani Geita kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti mwanafunzi mwenye umri wa miaka 8 baada ya kumrubuni kwa kumpa vizawadi vidogo vidogo ikiwemo kumnunulia chapati.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Adamu Maro amesema mpaka sasa jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa mtuhumiwa ambaye anadaiwa kutumia nafasi ya yeye kuwa kinyozi kutenda kosa hilo.

“Ushahidi wa daktari tayari umeshatoka na tayari tumeita mashahidi kadhaa kuweza kuwahoji walichoona. Jalada limeshakamilika na litapelekwa kwa mwanasheria na taratibu za kumpeleka mahakamani ziweze kukamilika mara moja,” amesema.

Kamanda Maro ametumia nafasi hiyo kukemea vitendo hivyo pamoja na kuwataka wanafunzi kuwaepuka wanaume wanaowarubuni kwa lifti, fedha na zawadi ndogo ndogo ili kuepuka vitendo vya ukatili kwa jamii.

Swahili Times imepata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya Kalangalala ambao wamelaani vikali kitendo alichofanyiwa mwanafunzi huyo huku wakiiomba serkali kuwachukulia hatua kali za kisheria wanaume wote wanaobainika kufanya ubakaji ili kuweza kukomesha vitendo hivyo.

Send this to a friend