Kiongozi wa Gabon atangaza kutopokea mshahara wa Urais

0
41

Kiongozi wa kijeshi wa Gabon, Jenerali Brice Oligui Nguema amesema hatapokea mshahara wake kama Rais na badala yake atapokea mshahara wake kama kamanda wa kijeshi.

Kwa mujibu wa msemaji wa Serikali ya kijeshi, Nguema ambaye ni rais wa mpito aliyeingia madarakani baada ya kupinduliwa kwa Rais Ali Bongo mwezi Agosti, amechukua hatua hiyo kutokana na mahitaji mengi ya watu wa Gabon.

Mbali na kutopokea mshahara wa urais, Jenerali Nguema pia ameamua kupunguza matumizi ya fedha za umma kwa kupunguza posho kwa wabunge, kuondoa fedha za kisiasa na kupunguza marupurupu ya vikao kwa lengo la kuimarisha hazina ya nchi.

Utawala wa miaka 14 wa Rais aliyeondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo, Ali Bongo ulikumbwa na madai mengi ya ufisadi na kashfa nyingine nyingi za kifedha.

Send this to a friend