Kiongozi wa kanisa afariki akiwa na mwanamke hotelini

0
46

Kasisi wa Kanisa Katoliki la Jimbo Kuu la Nairobi nchini Kenya ameripotiwa kufariki baada ya kupoteza fahamu katika hoteli moja kaunti ya Murang’a.

Kulingana na ripoti ya polisi, Fr. Joseph Kariuki Wanjiku (43) aliingia katika hoteli hiyo Ijumaa usiku akiandamana na mwanamke wa miaka 32 ambaye pia ni mfanyakazi mwenzake huko Ruai.

Inadaiwa mwanamke huyo aliwataarifu wasimamizi wa hoteli hiyo kwamba Kariuki amepata kizunguzungu na kupoteza fahamu na ndipo waliamua kumkimbiza hospitalini lakini alifariki dunia wakiwa njiani.

Polisi wamesema mwili wa Karuki ulikutwa ukiwa umefunikwa nusu kwenye chumba hicho huku povu jeupe likitoka mdomoni na puani.

Mwili huo umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Mater Hospital jijini Nairobi ukisubiri kufanyiwa uchunguzi na hatua zaidi za polisi.

Send this to a friend