Kipato cha kila mkazi wa Dar chaongezeka kwa laki 5

0
43

Takwimu zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonesha ongezeko la asilimia 5 katika wastani wa kipato cha Mtanzania kwa mwaka ambao umechagiwa na na kukua kwa uchumi wa Kanda ya Dar es Salaam, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa.

Takwimu zinaonesha kuwa wastani wa kipato cha Mtanzania (GDP per Capita) cha mmoja mmoja kimeongezeka zaidi kutoka wastani wa TZS milioni 2.7 hadi Shilingi milioni 2.8.

Wastani wa kipato cha wakazi wa Dar es Salaam kimeongezeka zaidi kuliko maeneo megine nchini kutoka Shilingi milioni 4.81 hadi shilingi milioni 5.39 kwa mwaka 2022 sawa na ukuaji wa asilimia 12 ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo kila mkazi wa Dar es Salaam aliongeza TZS 500,000 katika mapato yake ya mwaka .

Nchi 10 za Afrika zenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi 2023

Hata hivyo, hesabu ya pato la mtu mmoja mmoja inapatikana kwa kugawa pato la Taifa au eneo fulani (GDP) kwa idadi ya watu waishio humo.

Shirikia la Fedha Duniani (IMF) linasema GDP hupimwa kwa kuangalia thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa katika kipindi husika na pia si zote ambazo zinajumuishwa.

Send this to a friend