Kiswahili chatangazwa lugha rasmi Uganda

0
16

Baraza la Mawaziri la Uganda limeridhia uamuzi wa viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutumia Kiswahili kama lugha rasmi.

Akizungumza Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Mwangalizi wa nchi hiyo, Dkt. Chris Baryomunsi amesema Baraza la Mawaziri limependekeza kuwa, ni lazima Kiswahili kifundishwe katika shule za msingi na sekondari pamoja na somo hilo kufanyiwa mitihani.

“Pia ilikubaliwa kwamba, programu za mafunzo kwa bunge, Baraza la Mawaziri na vyombo vya habari kuhusu lugha hiyo ianzishwe,” amesema.

Tangu mwaka 1962 lugha rasmi Uganda ilikuwa ni Kiingereza na ilipofika mwaka 2017 kituo cha Maendeleo ya Mitaala cha Uganda [NCDC] kilihitimisha maandalizi ya mitaala kwa shule za sekondari, hivyo Kiswahili kikatangazwa somo la lazima kama ilivyo kwa kiingereza.

Send this to a friend