Kitambaa Cheupe, Wavuvi Kempu na nyingine 80 zafungiwa kwa kusababisha kelele

0
18

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limezifungia sehemu za starehe za wazi zaidi ya 80 baada ya kukuta kelele zinazoathiri wakazi wa maeneo hayo na biashara licha ya kupewa onyo na NEMC na wengine kupewa faini.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka amesema Sheria ya Usimamizi wa Mazingira namba 20 ya mwaka 2004 na Kanuni ya Viwango vya Udhibiti wa Kelele na Mtetemo ya mwaka 2015 imesema maeneo ambayo yanazunguka maeneo ya watu na kuna biashara, kelele zinapaswa kuwa 60 DBA wakati wa mchana, na usiku kuwa 40.

Ombi la Fei Toto lakataliwa tena TFF

Baadhi ya sehemu zilizofungiwa ni pamoja na Elements, Wavuvi Camp, Boardroom, Kitambaa Cheupe, Liquid, Warehouse na Soweto za Dar es salaam pamoja na Chako ni Chako, Rainbow, Gentleman za jijini Dodoma na The Cask ya Mwanza.

“Hawa tumechukua hatua hizo za kufunga kwa sababu sio mara ya kwanza kuwaonya tulishapita mara nyingi lakini hawakusikia, baada ya kuwafungia wengi wamefika kuomba msamaha na wengine wameomba wafunguliwe,” amesema.

Send this to a friend