Kitilya na wenzake wakimbilia mahakamani kupinga makubaliano na DPP

0
23

Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake wawili wamekimbilia mahakama ya Rufani kuomba kuruhusiwa kupinga makubaliano baina yao na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) yaliyowatia hatiani katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikiwakabili.

Kitilya, Shose Sinare na Sioi Solomon wamekata rufaa mahakamani hapo wakipinga uamuzi wa Mahakama Kuu iliyotupilia mbali maombi yao ya kuongezewa muda kufungua shauri la maombi ya kutengua hukumu iliyowatia hatiani.

Aidha, kwa mujibu wa wakili wao, Zaharani Sinare, hukumu hiyo ilitokana na makubalianao yasiyo halali baina yao na DPP wakidai yalifikiwa bila hiari yao.

Watatu hao na wenzao wengine wawili, Bedason Shallanda na Alfred Misana walitiwa hatiani na Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi namba 4 ya mwaka 2019 iliyokuwa ikiwakabili.

Walihukumiwa kulipa faini ya TZS milioni 1 kila mmoja na fidia ya TZS bilioni 1.5 kama walivyokubaliana baada ya majadiliano baina yao na DPP na ilipofika 2022 Kitilya na wenzake walifungua shauri la maombi ya kutengua hukumu hiyo.

Send this to a friend