Kituo cha afya Chikundi kuokoa maisha ya wananchi

0
35

Kwa muda mrefu wananchi wa Kata ya Chikundi, wilaya ya Masasi wamekuwa wakiishi na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo ya karibu kwani iliwalazimu kwenda mbalimbali na kutumia gharama kubwa huku wengine wakipoteza maisha kama wajawazito.

Moza Kaspari ni mmoja wa wahanga wa changamoto hiyo lakini sasa anamshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuweza kujenga kituo cha afya cha kata hiyo na kukiri kwamba sasa hawatapata tena shida na wajawazito watajifungua salama.

“Ukiwa na ujauzito kwenda Ndanda lazima ukodi gari ambalo ni shilingi 10,000 na ukichukua bajaji ni shilingi 6,000 , kwa kipindi chote tumekuwa tukiishi maisha hayo ya shida na ukifika kule gharama za matitabu ni kubwa sana kiasi kwamba watu wengine wanazalia nyumbani na kupoteza watoto,”

“Nina mshukuru Mama Samia, yani shukrani zangu ni za dhati na sio mimi tu wananchi wote wa tarafa hii na kata hii wanashukuru sana. Mimi kama mama nasema kweli mama yoyote akiwa kiongozi anakuwa na huruma na anaokoa maisha ya watu sio ya mtu mmoja, jamii yote mimi naamini hata na wapita njia watakuja kutibiwa hapa,” alisema Moza.

Send this to a friend