Kiwanda cha kutengeneza transfoma chazinduliwa Dar

0
14

Waziri wa Nishati, January Makamba amezindua kiwanda cha kuzalisha transfoma ikiwa ni awamu ya pili ya kiwanda cha kuzalisha vifaa vya umeme cha Elsewedy Electrica Industrial Complex kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Awamu ya kwanza ya kiwanda hicho inayohusisha utengenezaji wa nyaya za umeme ilizinduliwa Desemba 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza wakati wa uzinduzi leo Septemba, 2022 Waziri Makamba amepongeza uwekezaji huo na kueleza Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji.

“Ni mafanikio makubwa kuona awamu ya pili ya kiwanda inakuja ikiwa ni miezi sita tu tangu kuanza kwa uzalishaji wa awamu ya kwanza,” amesema.

Waziri Makamba ameongeza, “hii inaonyesha kiasi gani mmedhamiria kufanya uwekezaji wenye tija. Upande wetu Serikali tutaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa biashara.”

Aidha, awamu ya pili ya kiwanda hicho ambayo inahusisha uzalishaji wa transfoma kina uwezo wa kuzalisha trasfoma 2,500 kwa mwaka na kikitarajiwa kutengeneza ajira 1500.

Send this to a friend