Kiwanda cha kuzalisha bangi Rwanda kukamilika Septemba

0
110

Ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha bangi katika Mji wa Musanze uliopo Kaskazini mwa Rwanda unatarajiwa kukamilika katika wiki ya kwanza ya mwezi Septemba, mwaka huu .

Kituo hicho kinajengwa na kampuni ya King Kong Organics (KKOG) Rwanda, kampuni tanzu ya shirika la Marekani la KKOG Global, ambalo mwezi Machi mwaka huu lilipata leseni ya miaka mitano kutoka kwa serikali ya Rais Paul Kagame ya kuzalisha bangi.

Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB) iliidhinisha kampuni hiyo kulima bangi kwa madhumuni ya dawa. Mimea ya bangi hukua baada ya miezi minne hadi sita na KKOG inataka kuzalisha angalau kilo 5,000 za bangi kwa hekta.

“Tuko katika asilimia 70 kukamilisha kituo hicho na tunatarajia kukamilika kufikia wiki ya kwanza ya Septemba,” Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa KKOG Rene Joseph alisema.

Rais Samia kuwagharamia walioshindwa kupandikiza figo

Kampuni hiyo imesema imemwaga dola milioni 10 (TZS bilioni 27) katika ununuzi wa mashine, ujenzi wa kituo, malipo ya ada katika ununuzi wa ardhi na wakandarasi, na kuagiza mbegu za bangi zilizobadilishwa vinasaba.

Maafisa wanakadiria kuwa hekta moja ya bangi inaweza kuzalisha hadi dola milioni 10 [TZS bilioni 27], ambayo ni mara 30 zaidi ya $300,000 [TZS milioni 810] ya hekta moja ya maua.

Send this to a friend