Kiwango cha maambukizi ya Malaria chapungua nchini

0
40

Wizara ya Afya imesema kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria nchini kimepungua na kufikia asilimia 8.1 kwa mwaka 2023 kutoka asilimia 15 kwa mwaka 2015.

Ameyasema hayo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha tathimini ya jitihata zilizofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau kupunguza maambukizi ya Malaria nchini, ambapo amesema kupungua kwa kiwango hicho ni kutokana na jitihada za Serikali katika kuhakikisha kiwango cha malaria kinafikia sifuri na kuweka mikakati ya kutokomeza mazalia ya mbu.

“Serikali kupitia wizara ya afya ikishirikana na wadau wa sekta ya afya imeweka dhamira ya kuhakikisha kiwango hiki cha Malaria kinapungua kabisa na kufikia ziro kwa sababu Tanzania bila Malaria inawezekana kwa kuwa na mikakati inayotekelezeka na kutoa elimu kwa jamii juu ya kudhibiti mazalia ya mbu wanaoambukiza Malaria katika makazi yao,” amesema Dkt. Jingu.

Marubani wasinzia kwa dakika 28 ndege ikiwa angani

Aidha, ametaja mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Songwe, Manyara, Kilimanjaro, Singida na Mwanza kuwa ni mikoa inayofanya vizuri kupunguza kiwango cha maambukizi ya Malaria kufikia asilimia 1, huku akitaja mikoa ya Katavi, Tabora na Kagera kuwa bado ina changamoto ya kiwango kikubwa cha maambukizi ya ugonjwa huo kutokana na hali ya kimazingira ya mikoa hiyo.

Send this to a friend