Kizz Daniel akamatwa na Polisi

0
43

Msanii maarufu kutoka nchini Nigeria, Kizz Daniel amekatwa na Polisi kutokana na kutotumbuiza katika tamasha la ‘Summer Amplified’ lililofanyika Jumapili 7, 2022 katika ukumbi wa NextDoor Arena, jijini Dar es Salaam.

Polisi wamefika katika hoteli aliyofikia msanii huyo kisha kumpakia katika gari la polisi pamoja watu wake na kumpeleka katika kituo cha polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam.

Str8up waomba radhi kutoonekana kwa Kizz Daniel

Mwanamuziki huyo hakutumbuiza katika tamasha alilotakiwa kutumbuiza usiku wa kuamkia leo, hivyo kupelekea wahudhuriaji waliolipa viingilio kufanya vurugu.

Tetesi zinadai kuwa hakutumbuiza baada ya kusahau begi lake la nguo nchini Kenya, na hivyo akakataa kuvaa nguo nyingine alizoletewa.

Kizz Daniel ni mmoja wa wasanii wanaofanya vizuri duniani na kwa sasa, ambapo anatamba na kibao chake cha ‘buga’ ambacho hivi karibuni ametoa maana ya neno hilo kuwa ni ‘sherehe’.

Send this to a friend