Kocha Ruvu Shooting afungiwa kwa kuwatukana Azam TV

0
37

Kocha msaidizi wa Klabu ya Ruvu Shooting, Renatus Shija ametozwa faini ya TZS milioni moja kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano na mtangazaji wa televisheni ya mdhamini mwenye haki za matangazo ya televisheni, Azam TV.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)  baada ya kikao kilichofanyika Aprili 15, 2023 ili kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufanyia maamuzi.

Nchi 10 za Afrika ambazo watu wake wana furaha zaidi

Kamati imesema kocha huyo alikataa mahojiano baada ya kumalizika kwa mechi ya Tanzania Prison waliofunga magoli 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting.

Aidha, Kocha Renatus amefungiwa michezo mitatu na kutozwa mfaini ya TZS milioni moja kwa kosa la kuwatolea lugha ya matusi wafanyakazi wa Azam TV ambao walikuwa wakijaribu kumsihi akubali kufanya mahojiano hayo.

Send this to a friend