Kocha Sven: Mo Dewji na Barbara walinishawishi sana nibaki

0
41

Aliyekiwa Kocha Mkuu wa Simba SC, Sven Vandebroeck amesema kuwa ameachana na klabu hiyo ili kupata uwiano wa muda sawa kati ya kazi, familia pamoja na maendeleo yake binafsi.

Sven amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na jumbe mbalimbali za kuagwa alizotumiwa baada ya kuondoka klabuni hapo.

“Ninamshuruku sana rais MO na CEO Barbara kwa utendaji wao wa kitaalamu na kunisaidia kufanya kazi zangu. Wote wawili walinishawishi hadi dakika ya mwisho nibaki,” ameeleza Sven.

Katita taarifa yake, Simba SC iliwaeleza wanachama na mashabiki wake kuwa imefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu.

Hatua hiyo ilikuja siku moja baada ya klabu hiyo kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuiondoa FC Platnum kwa jumla ya magoli 4-1.

Kufuatia hatua hiyo, Kocha Msaidizi, Selemani Matola anakaimu nafasi hiyo hadi hapo kocha mpya atakapopatikana.

Send this to a friend