Kocha wa Taifa Stars afungiwa na CAF

0
64

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemfungia kocha wa Taifa Stars, Adel Amrouche mechi nane kufuatia kauli zake kuwa Morocco inaushawishi ndani ya CAF katika kupanga mechi pamoja na waamuzi.

Katika taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) imesema adhabu hiyo ilitolewa jana na Kamati ya Nidhamu ya CAF baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (RMFF) kuwasilisha malalamiko dhidi yake.

Aidha, Kamati ya Utendaji ya TFF imemsimamisha kocha huyo na kumteua Hemed Morocco kuwa kaimu kocha ambaye atasaidiwa na Juma Mgunda.

Taifa Stars ni miongoni mwa nchi 24 zinazoshiriki mashindano ya 34 ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) huku ikiwa kundi moja na DR Congo, Zambia, na Morocco.

Send this to a friend