Kocha wa Taifa Stars aondolewa

0
46

Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) limefikia makubaliano ya kumuondoa Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen kwenye benchi la ufundi pamoja na wasaidizi wake.

Pousen ataendelea kubaki kuwa kocha katika timu za Taifa za vijana mpaka pale mkataba wake utakapomaliza rasmi.

TFF imeeleza kuwa kwa wakati huu benchi la ufundi la Taifa Stars litakuwa chini ya kocha Hanour Janza akisaidiwa na Meck Maxime pamoja na kocha wa magolikipa, Juma Kaseja.

Cesar Manzoki atimkia China

Agosti 28, 2022 Tafa Stars ilipoteza mchezo wake dhidi ya Uganda kwa kufungwa goli 1-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu CHAN katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Send this to a friend