Kombe la Muungano kurejea baada ya miaka 20

0
94

Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimetangaza kurejea rasmi kwa Kombe la Muungano baada ya miaka 20 kupita.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo imesema timu za Simba SC na Azam FC kutoka Bara zitashiriki mashindano ya mwaka huu yenye sura ya uzinduzi wa kombe hilo, huku kwa upande wa Zanzibar, timu shiriki zikiwa KMKM pamoja na KVZ FC.

Aidha, mechi hizo zitachezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia Aprili 23, mwaka huu.

Send this to a friend