Kongamano la kumbukizi ya Hayati Mkapa kufanyika Zanzibar

0
72

Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF) kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeandaa kongamano la kumbukizi ya maisha ya Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa litakalofanyika ikiwa ni siku chache kabla ya siku ya kumbukizi ya kifo cha Mkapa Julai 23.

Katika kongamano hilo litakalofanyika kwa siku mbili Julai 13 na 14 katika hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar, linatahudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Makamu wa kwanza wa Rais, Othman Masoud.

Dar es salaam jiji la sita kwa usafi Afrika

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Mtendaji Mkuu wa BMF, Dk Hellen Senkoro amesema kongamano hilo la pili tangu kufariki kwa Mkapa mwaka 2020, litahudhuriwa pia na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi akiwemo Rais mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chissano.

“Mijadala itakayofanyika siku ya kwanza itahusu mada kuu mbili ambayo ni kuongeza kasi katika mikakati ya mabadiliko ya sekta ya afya Tanzania kupitia ushirika wa kibiashara na sekta binafsi,” amesema.

Mada nyingine itahusu ubunifu katika mikakati ya ushirikiano kati ya taasisi za Serikali na taasisi binafsi katika kufikia lengo la kutoa huduma ya afya kwa wote.

Kauli mbiu ya kongamano hilo inasema ‘Urithi kutoka kwa Mkapa: Uongozi shupavu katika kuchochea mabadiliko kwa wote.’

Send this to a friend