Korea Kaskazini kufunga ubalozi wake nchini Uganda

0
42

Korea Kaskazini inatarajia kufunga ubalozi wake nchini Uganda kufuatia mkutano kati ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na balozi wa Korea Kaskazini, Jong Tong Hak siku ya Jumatatu.

Taarifa kutoka Ikulu ya Uganda iliyonukuliwa na shirika la habari la AFP imesema “Balozi Jong amemwambia Rais kwamba Korea Kaskazini imechukua hatua ya kimkakati ya kupunguza idadi ya balozi zake Afrika, ikiwa ni pamoja na Uganda, ili kuongeza ufanisi wa taasisi za nchi hiyo nje ya nchi.”

“Urafiki wetu mzuri utaendelea na utazidi kuimarishwa na kukuzwa,” amesema Balozi Jong.

Korea Kaskazini ilianzisha uhusiano na Uganda muda mfupi baada ya nchi hiyo kupata uhuru kutoka Uingereza mwaka 1962.

Tanzania yatenga hekta 20 Bandari Kavu ya Kwala kwa ajili ya Zambia

Mji wa Pyongyang ulimuunga mkono Idi Amin alipochukua madaraka mwaka 1971, ikitoa mafunzo na silaha kwa vikosi vyake na kisha Korea Kaskazini ikafungua ubalozi wake mwaka mmoja baadaye.

Send this to a friend