Korea Kusini yatumia trilioni 466 ili kuongeza idadi ya watu

0
31

Korea Kusini hivi majuzi ilivunja rekodi ya kuwa na kiwango cha chini zaidi cha uzazi duniani. Takwimu zilizotolewa zimeonesha wastani wa idadi ya watoto ambao mwanamke wa Korea Kusini atakuwa nao katika maisha yake ni chini ya hadi kiwango cha 0.79 tu ambapo kawaida ingepaswa kuwa na kiwango cha 2.1.

Kiwango cha kuzaliwa kwa Korea Kusini kimekuwa kikishuka tangu 2015, na mnamo 2020 nchi hiyo ilirekodi vifo vingi zaidi kuliko waliozaliwa na jinsi viwango vya uzazi vinapozidi kupungua, wanawake wa Korea Kusini pia wanapata watoto wakiwa na umri mkubwa.

Umri wa wastani wa wanawake waliojifungua mnamo 2021 ulikuwa zaidi ya miaka 33.4 kuliko mwaka uliopita, kulingana na takwimu huku idadi ya wazee ikiongezeka.

Wataalam wanahofia hali hiyo itaiacha nchi hiyo ikiwa na watu wachache wa umri wa kufanya kazi ili kusaidia idadi ya wazee inayozidi kuongezeka kwa kulipa kodi pamoja na huduma mbalimbali.

Kufikia Novemba mwaka jana, asilimia 16.8 ya Wakorea Kusini walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 65, wakati asilimia 11.8 tu walikuwa na umri wa miaka 14 au chini ya hapo.

Nchini Korea Kusini na Japan kuna sababu sawa za kupungua kwa watoto wanaozaliwa ikiwa ni pamoja na kiwango cha chini cha mishahara, kupanda kwa gharama za maisha na kupanda kwa bei ya nyumba.

Wanawake wengi wa Korea Kusini wanasema hawana muda, pesa, au uwezo wa kihisia wa kuchumbiana huku wakiweka taaluma yao kwanza katika soko la kazi lenye ushindani mkubwa ambapo mara nyingi wanakabiliana na mfumo dume na ukosefu wa usawa wa kijinsia.

Rais wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol alikiri katika ziara yake kwamba zaidi ya dola bilioni 200 [TZS trilioni 466] zimetumika kujaribu kuongeza idadi ya watu katika kipindi cha miaka 16 iliyopita.

Hata hivyo tangu kushika wadhifa wake, utawala wake haujatoa majawabu ya kutosha juu ya kusuluhisha tatizo hilo isipokuwa kuendelea na njia ya kuunda kamati ya kujadili suala hilo na kuahidi msaada zaidi wa kifedha kwa watoto wachanga.

Pia, posho ya kila mwezi kwa wazazi walio na watoto hadi mwaka 1 itaongezeka kutoka takribani TZS laki 537 hadi TZS milioni 1.2 mnamo 2023 na hadi takribani TZS milioni 1.8 ifikapo 2024, kulingana na utawala wa Yoon.

Serikali ya Korea Kusini imeanzisha hatua kadhaa katika miaka ya hivi karibuni ili kukabiliana na kushuka kwa kiwango cha uzazi, ikiwa ni pamoja na kuruhusu wazazi wote wawili kuchukua likizo ya uzazi kwa wakati mmoja na kuongeza muda wa likizo ya malipo kwa mwanaume.

Send this to a friend