Korea kuwalipa milioni 1 kila mwezi vijana wanaosumbuliwa na upweke

0
65

Korea Kusini imetangaza kutoa $500 [TZS milioni 1.17] kila mwezi kwa kila kijana anayepitia hali ya upweke na kujitenga kwa lengo la kuboresha afya zao za akili na udumavu wa mwili pamoja na kuwahimiza kuungana tena na jamii yao.

Wizara ya Usawa wa Jinsia na Familia ya nchini Korea Kusini imesema hatua hiyo mpya ina lengo la kuwafanya vijana waliokata tamaa na kujitenga wenye umri wa miaka tisa hadi 24 kurejea tena shuleni, kutafuta kazi na kurudi katika maisha yao ya kila siku.

Msemaji wa wizara ameiambia Insider kuwa Serikali italipa kiasi hicho cha pesa kupitia akaunti ya benki ya vijana, na walioko chini ya umri wa miaka 18, pesa hizo zitatumwa katika akaunti za wazazi wao au walezi kwa idhini yao.

Kenya yakodi ardhi ya kulima mahindi nchini Zambia

“Pia hawatalazimika kuthibitisha kuwa wanatoka nje ili kuendelea kupokea pesa hizo,” msemaji huyo ameongeza.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2022 kutoka Taasisi ya Korea ya Afya na Masuala ya Kijamii, takribani watu 338,000 wenye umri wa kati ya miaka 19 na 39 nchini humo wamekuwa wakisumbuliwa na upweke, hivyo kujifungia nyumbani kwa muda mrefu, wakikwepa shule na kufanya kazi kwa miezi au hata miaka.

Send this to a friend