Korea yaahidi kuiunga mkono Tanzania katika Sekta ya Maji

0
6

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (Mb) ametembelea na kufanya mazungumzo na Benki ya EXIM ya Korea ambayo imetoa fedha za utekelezaji wa miradi ya majitaka nchini Tanzania yenye jumla ya Dola za Kimarekani milioni 248.3 (Dar es Salaam dola milioni 90, Dodoma dola milioni 70 na Iringa dola milioni 88.3).

Makamu wa Rais wa Benki hiyo amesema kupitia EDCF na Mifuko mingine, Serikali ya Korea itaendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania kupitia Sekta ya Maji katika uwekezaji zaidi wa utekelezaji wa miradi ya maji.

Utelezaji wa miradi hiyo unatajwa kuimarisha huduma za usafi wa mazingira, kuondoa na kutibu majitaka. Vilevile, Tanzania imepata msaada wa Dola za Kimarekani milioni 8 ambazo zitajenga mfumo wa kusimamia huduma za maji (Smart Water Management System) katika Mamlaka ya Maji Iringa kutoka Korea Environmental Industry and Technology Institute (KEITI).

Pia, Kupitia mfumo huo, IRUWASA itakuwa Mamlaka ya Maji ya kwanza nchi kutumia mfumo huo ambao utaongeza ufanisi katika kudhibiti upotevu wa maji, kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuimarisha huduma ya maji.

Kupitia ziara hiyo, Aweso ameimarisha ushirikiano na wadau wa maji nchini Korea ambao ni K-Water na makampuni mbalimbali, hali ambayo imefungua fursa zaidi za kushirikiana katika kujengea uwezo watumishi na Taasisi za Maji ikiwa ni pamoja na kuandaa miradi na kutafuta fedha.

Send this to a friend