Korea yaipa Tanzania mkopo wa bilioni 427 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali Zanzibar

0
62

Serikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Korea zimesaini Mkataba wa Mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 163.6 [TZS bilioni 427.8] kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni, iliyopo Zanzibar pamoja na kituo cha mafunzo ya utabibu.

Mkataba wa Mkopo huo umesainiwa jijini Soeul Juni 05, 2024 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na kwa upande wa Korea umesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi na Mjumbe wa Bodi wa Benki ya Exim ya Korea, Hwang Kiyeon.

Balozi Togolani akanusha Tanzania kusaini mkopo Korea Kusini unaohusisha sehemu ya bahari

Ujenzi wa Hospitali hiyo utahusisha majengo ya Hospitali yenye vitengo vinne vya magonjwa Maalum kama ya kina mama na watoto, Kituo cha Mafumzo, nyumba za makazi kwa wafanyakazi, ununuzi na ufungaji wa vifaa vya matibabu vya teknolojia ya kisasa na usimikaji wa mfumo wa afya wa mawasiliano.

Mkataba huo wa mkopo umetiwa saini wakati Rais Samia Suluhu Hassan akiendelea na ziara yake ya siku sita nchini Korea.

Send this to a friend