Kubenea akamatwa na fedha za kigeni akiingia nchini

0
38

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imemfungulia kesi aliyekuwa mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea ambapo anakabiliwa na tuhuma za kuingia nchini Tanzania na kuingiza nchini fedha za kigeni kinyume na sheria.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka, Bwisalo Mganga inaeleza kuwa Septemba 5 mwaka huu mtuhumiwa alivuka mpaka usio rasmi na kuelekea Nairobi, Kenya, na kisha kurejea Tanzania bila kutumia mpaka rasmi.

Pia, mtuhumiwa aliingiza nchini fedha za kigeni bila kutoa tamko rasmi la kisheria kinyume na masharti ya Kanuni za Sheria ya Kuzuia Utakatishaji Fedha Haramu Na. 12 ya mwaka 2006.

Bwisalo amesema mtuhumiwa alikutwa na fedha za kigeni ambazo ni dola za Marekani 8,000 na shilingi za Kenya 491,700.

Mtuhumiwa alipohojiwa alisema kuwa alifika mkoani Arusha Septemba 2, 2020 akitokea Dar es Salaam na kufikia katika hoteli. Alieleza kuwa tarehe 3 alienda kulala kwa kakaye na tarehe 4 alienda Namanga kupokea fedha tajwa hapo juu pamoja TZS 71,000 kutoka kwa raia wa Kenya.

Hata hivyo taarifa ya ofisi hiyo imeeleza kuwa ushahidi umeonesha maelezo ya Kubenea si ya kweli.

Send this to a friend