Kuchangia earphones kunaweza kusababisha ukiziwi

0
45

Utafiti unaonesha matumizi ya kuchangia spika za masikio yaani ‘earphones’ husababisha maambukizi ya magonjwa yanayotokana na vijidudu kwa njia ya masikio.

Akizungumza Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke, Dar es Salaam, Dokta Jabiri Kunamba amesema moja ya athari za kuchangia ‘earphones’ ni pamoja na kupata magonjwa ya ngozi.

“Kundi kubwa la wanafunzi na wafanyakazi, wako katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa ya masikio kutoka na mazoea ya kuchangia matumizi ya ‘earphones’ bila kujali afya zao,” amesema daktari huku akibainisha kuwa wagonjwa wengi huwa na maambukizi kwenye ngoma ya sikio yanayotokana na kuchangia ‘earphones.’

Amesema madhara ni makubwa kwa kuwa masikio yako karibu na ubongo hivyo huenda mtu akapata maambukizi kupitia mishipa na hivyo kupata madhara zaidi kama kupata ukiziwi, kupoteza nguvu ya kuona na matatizo ya uti wa mgongo.

Chanzo: Uhuru

Send this to a friend