Kuhusu madai ya wananchi kuuawa, Spika Tulia aipa serikali miezi mitatu

0
52

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, amepokea ushahidi kutoka kwa wabunge wawili aliowaagiza Juni 3 mwaka huu kuleta uthibitisho kwa kile walicholalamika kuhusu wananchi wa majimboni mwao kuuawa.

Dkt.Tulia amesema Jumatatu Mbunge Tarime Vijijini, Mwita Waitara alidai kuwa baadhi ya wananchi wake wameuawa kwa kipigwa risasi na maafisa wanyamapori na kuchukuliwa mifugo yao.

Naye Mbunge wa Songwe, Philip Mulugo alidai wananchi wa jimbo lake waliuawa na Tembo, Simba na Mamba, hivyo kumpelekea Dkt.Tulia kuwataka wafikisha uthibitisho wa madai yao mezani kwake.

Dkt. Tulia amesema taarifa zao wabunge hao hazina uthibitisho wa kutosha badala yake ni malalamiko yaleyale ya wananchi ambayo wabunge hao walichangia kwenye bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Aidha, Spika ameiagiza Serikali kufuatilia malalamiko hayo na kufanya uchunguzi wa kutosha ndani ya miezi mitatu ili bunge lipate taarifa juu ya uhalisia wa jambo hilo.

Send this to a friend