Kukua kwa teknolojia ya mawasiliano kunavyochangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi Tanzania

0
38

Na Bindu Hassan,UDBS

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Zainab Chaula wiki hii ameeleza namna sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) inavyoweza kuchangia zaidi katika ukuaji wa sekta za kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.

Dkt. Chaula ameeleza kuwa huduma za mawasiliano zimekuwa muhimu sana katika maendeleo na kwamba imechangia Tanzania kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa kati (lower-middle-income status).

Kauli ya kiongozi huyo inaonesha namna maendeleo katika sekta ya mawasiliano, ikijumuisha matumizi ya simu za mkononi na matumizi ya intaneti, zimekuwa muhimu katika kuchagiza maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Hakika, tangu mwaka 2016 na kutungwa kwa Sera ya Taifa ya Habari na Mawadiliano (National Information and Communications Technology Policy), Tanzania imeshuhudia wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na idara za serikali, washirika wa maendeleo na watoa huduma wa mawasiliano ya simu wakija pamoja na kushirikiana kwa karibu kutumia fursa mbalimbali za kidijitali zinazojitokeza.

Mfano hai wa hili ni kazi za watoa huduma za simu kama Tigo Tanzania. Pamoja na kuwa kinara katika sekta hiyo, Tigo imekuwa ikihakikisha inakuwa mshirika hai katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

Ukiangazia sekta ya afya kama mfano, huduma ya usajili wa vizazi hai ya Tigo inawapa fursa wazazi kusajili taarifa za kuzaliwa kwa watoto wao kwa kuwaunganisha na huduma ya kimtandao kutoka serikalini. Pia, huduma ya bima ya afya ya Tigo (Tigo Bima Mkononi) imewasaidia wateja wake kupata aina mbalimbali za bima za afya wanazotoa.

Katika miaka ya hivi karibuni, Tigo imekuwa na mchango mkubwa sana katika miradi kwenye ngazi ya jamii. Hii inajumuisha kuchimba visima vya maji vijijini na kuhakikisha jamii zinapata maji safi.

Kwingineko, Tigo imekuwa ikishirikiana na taasisi nyinginezo kutoa ujuzi muhimu wa teknolojia kwa wasichana, ili waweze kutumia ujuzi huo kupata ajira na kuendeleza taaluma zao.

Taarifa iliyotolewa mwaka jana kuwa Tigo na Zantel zinakusudia kuungana ni taarifa nyingine nzuri kwa sekta hiyo.Kwa kuunganisha uendeshaji wao na miundombinu, kampuni hizo zitakuwa na uwezo mkubwa wa kuratibu mapinduzi ya kidijitali nchini Tanzania, ambapo pia itatoa fursa ya kuwezesha mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.

Tukumbuke kazi kubwa ya sekta hii, na kwa pamoja tutegemee mambo bora zaidi yajayo.

Send this to a friend