Kula vyakula hivi kuepuka kupata upara

0
16

Tatizo la kupungua kwa nywele na kuwa na kipara limekuwa likiwatatiza wanaume wengi. Shida hii mara nyingi huaanza wanaume katika umri wa miaka 30, na kufikia umri wa miaka 50, wanaume huwa wanakabiliwa na tatizo hili.

Wengi wamekuwa wakitafuta namna mbalimbali za kukabiliana na hali hii, baadhi wakitumia dawa za kisasa na wengine za kiasili lakini ufanisi wake huwa tofauti.

Wanaume hasa katika mataifa yaliyoendelea hufanyiwa upandikizaji wa nywele japo kuwa gharama yake huwa juu mno inayogharimu kuanzia TZS milioni 2.8 hadi TZS milioni 83.

Kuna ushahidi kwamba aina fulani ya vyakula vina uwezo wa kuzuia upara. Utafiti umeonesha kwamba ulaji wa vyakula vyenye Omega 3 kama nyama na Samaki kwa wingi ulipunguza kupungua kwa nywele.

Lakini pia upara huhusishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini, hivyo kula vyakula vyenye madini ya chuma kama vile spinachi, kunde, maini, dagaa na kadhalika kunaweza pia kusaidia kutopoteza nywele zako.

Mbali na kula vyakula vifaavyo, utafiti unaeleza pia kwamba kufanya mazoezi zaidi na kupunguza mawazo ni mambo yanayoweza kupunguza kunyonyoka kwa nywele pia.

Mbali na hayo jaribu kuosha nywele zako kila siku kwa shampoo laini kwani inasaidia kuondokana na uwezekano wa uharibifu wa nywele kwa sababu ya dandruff au ukosefu wa usafi.

 

Send this to a friend