Kumbukizi: Ndege iliyokuwa imembeba Mama Teresa inapata ajali Tabora na kuua watano
Oktoba 11, 1986 ndege ndogo iliyokuwa imembeba Mama Teresa iliacha njia na kuparamia watu waliokuwa pembeni na kupelekea vifo vya watu watano na majeruhi.
Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na Clarapia, mtawa mwenye asili ya India kutoka kituo cha Hombolo cha Mama Teresa chakusaidia wenye mahitaji (Hombolo Missionary Center) kilichopo mkoani Tabora.
Wengine ni watoto wawili wa kiume wenye umri wa miaka 12 na 14, na wanaume wawili ambao mmoja wao alikuwa akiendesha kituo hicho cha kusaidia wahitaji.
Taarifa ya Radio Tanzania ilieleza kuwa ndege hiyo iliyokuwa imembeba Mama Teresa na abiria wengine wawili ilishindwa kuruka na kuelekea walipokuwa wamekusanyika watu. Taarifa kutoka Dodoma zilieleza kuwa vifo hivyo vilitokana na watu hao kujeruhiwa na mapanga ya injini za ndege hizo.
Mama Teresa mwenye asili ya Alabania alishinda Tuzo ya Nobel mwaka 1979 kutokana na kujitoa kwake kuwasaidia watu wenye mahitaji kwenye kituo chake cha Calcutta na maeneo mbalimbali duniani.
Alitembelea Tanzania akitokea nchini Sudan.