Kundi la Sauti Sol latangaza kutengana

0
42

Kundi la wanamuziki maarufu nchini Kenya lilioshinda tuzo nyingi, Sauti Sol, limetangaza ziara ya kimataifa ya kuwaaga mashabiki kabla ya kutengana kwa muda.

Katika taarifa yake Jumamosi, kundi hilo limesema hatua hiyo itaanza kutekelezwa baada ya ratiba ya ziara yao ya kimataifa itakayowakutanisha katika mataifa mbalimbali barani Ulaya na Marekani.

“Tunafuraha kuwatangazia Sauti Sol, wakali wa muziki barani Afrika, wataanza ziara ya kutumbuiza katika miji 5 kote Marekani na kufuatiwa na vituo 10 barani Ulaya na vituo 4 nchini Canada kabla ya kupumzika kwa muda usiojulikana,” imesema taarifa hiyo.

Albamu 10 za Hip-hop zilzouzwa zaidi ulimwenguni

Kundi hilo limeeleza kuwa ziara hiyo itawapa fursa mashabiki kufurahia onesho la kipekee kutoka kwa kundi hilo kwa mara ya mwisho kabla ya kuacha kuimba pamoja kwa muda usiojulikana.

Aidha, wameeleza kuwa urafiki wao walioutaja kuwa na zaidi ya miaka ishirini utaendelea kuwa na nguvu huku wakieleza kuwa “wakati kutengana huku kwa muda kuna ashiria mwisho wa ukurasa maalum, pia inawakilisha mwanzo mpya wa Sauti Sol.”

Send this to a friend