Kunguni wasababisha wananchi kuuza samani zote za ndani

0
65

Baadhi ya wakazi wa eneo la Eastlands jijini Nairobi wamelazimika kuuza samani zao zote za ndani ili kujaribu kuzuia kunguni ambao wamekuwa kero kubwa.

Baadhi ya vitu vya nyumbani vimekuwa vikitupwa na vingine kuuzwa kwa wauzaji samani za mitumba zikiwemo vitanda, seti za sofa, kabati la nguo, viatu na magodoro na hivyo kufanya baadhi ya maduka hayo kujaa samani zilizojaa kunguni na kuziuza kwa bei nafuu.

Sherryl Magambo, mmoja wa wakazi wa eneo hilo amesimulia kwamba, aliamua kuuza samani zake zote baada ya kunguni kusambaa katika nyumba yake ya vyumba viwili.

Adaiwa kumuua mtoto ili kulipiza kisasi kwa mama yake

“Nilijaribu kila aina ya dawa, lakini kunguni waliendelea kuongezeka, na sikuweza kuvumilia tena. Niliona aibu hata kualika wageni nyumbani kwangu kwa sababu sebule hiyo ilikuwa na wadudu. Wadudu hao walisambaa katika chumba changu cha kulala, chumba cha wageni, na sebule yangu. Niliamua tu kuuza kila kitu kwa muuzaji wa mitumba, kwa bei nafuu sana,” amesema.

Wakati huo huo, wafanyabiashara wa samani za mitumba wanahifadhi na kufaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na usambazaji wa bei nafuu huku wateja wao wakiwa vijana wanaoanza maisha.

Send this to a friend