Kusogeza mtandao wa intaneti kwa Watanzania wengi zaidi kutakuza Pato la Taifa

0
43

Kwa sasa, zaidi ya asilimia sitini ya Watanzania wanaishi vijijini. Hata hivyo, jamii nyingi za wanaoshi vijiji bado zinaonekana kukosa huduma na fursa sawa na zinazofurahiwa na wenzao waishio mijini. Kwa mfano maeneo ya mjini yamekuwa na huduma bora za mawasiliano ya simu, ikiwa ni pamoja na huduma za intaneti. Wakati mwingine watu wa vijijini hukosa huduma hizi kutokana na maeneo yao kutofikika kiurahisi ili kuwezesha ujenzi wa miundombinu kama vile minara ya simu.

Hata hivyo, serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi imejikita kuhakikisha kuwa huduma hizo zinawafikia watu wote bila kujali eneo ambalo mhusika yupo. Pande zote mbili zinatambua kuwa, kwa kuwafikia watu wote na huduma za intenti kutawezesha kukuza Pato la Taifa lakini pia kutengeneza fursa mpya za ajira.

Kuna namna mbalimbali zinazoweza kutumika kupanua wigo wa huduma za intaneti maeneo ya vijijini.

Mfano wa njia moja ambao tayari umeanza kutekelezwa nchini Tanzania ni makampuni ya mawasiliano ya simu kushirikiana miundombinu kama vile minara.

Kwa mfano mwaka 2016 kampuni tatu, Tigo, Airtel na Vodacom zilishirikiana kuendeleza vituo sita vya intaneti (mobile broadband) ambavyo vingewezesha kutoa huduma ya intaneti kwa jumla ya wateja wa vijijini 72,000.

Kwa kuunganisha nguvu, watoa huduma pamoja na serikali waliweza kupanua kwa kiasi kikubwa miundombinu ya mawasiliano. Huduma hiyo imekuwa ya mafanikio sana. Huduma hiyo imeweza kuwafikia asilimia 95 ya wateja walengwa ambapo wengi wao wameisifia kuwa ni bora.

Namna nyingine bora ya kupanua huduma hiyo ni kubadili mfumo wa soko kwa kuunganisha kampuni husika. Kwa kuungana kampuni, zitaweza kutoa huduma bora na kwa ufanisi zaidi pamoja na kukuza uwekezaji. Hii itasaidia zaidi kwenye kuwekeza katika huduma na upanuzi wa teknolojia, ikiwa ni pamoja na katika maeneo ya vijijini.

Kampuni mbili tayari zimeeleza kusudio la kutaka kuungana. Tigo Tanzania pamoja na Zantel zinaripotiwa kuwa sasa zipo katika hatua za mwisho mwisho za kuungana, hatua ambayo itaimarisha sekta hiyo nchini kote.

Akizungumzia hatua hiyo katika makala iliyochapishwa na Forbes, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo alieleza kuwa kwa namna gani kuungana kwa kampuni hizo kutaongeza ubora wa huduma zitolewazo pamoja na kusaidia ongezeko la wateja.

Makala hiyo pia iligusiwa na viongozi wa upande wa Zantel, ambao walisema kuwa kampuni zao zinaungana na kuja kwa pamoja kwa lengo kubwa la kufanikisha mandeleeo ya Tanzania na watu wake.

Wakazi wa vijiji wameanza kufurahia matunda ya makampuni ya simu kuanza kushirikiana kwenye minara. Hii inaashiria kuwa manufaa ya kuimarisha soko kwa kuungana yatakubwa makubwa na yapo karibuni.

Send this to a friend