Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikaeli Mbowe.
Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki.
“Tanzania hii ni yetu, wote tunatakiwa kushirikiana kuijenga Tanzania.”- Rais Samia Suluhu Hassan pic.twitter.com/FScqRLuGBS
— Swahili Times (@swahilitimes) March 4, 2022
Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuonesha kwake kujali huku akikubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga taifa la Tanzania ni kusimama katika haki.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema wapo tayari kumpa Rais Samia Suluhu ushirikiano ili ndani ya nchi pawe na furaha ambayo ameanza kuijenga. pic.twitter.com/7c33gqJE9P
— Swahili Times (@swahilitimes) March 4, 2022
Vile vile, amesema wamekubaliana kufanya siasa za kistaarabu na za kiungwana na kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ili nao pia waweze kutekeleza majukumu yao ipaswavyo.