Kuungana kwa makampuni ya simu kutaimarisha uchumi wetu

0
38

Na John Akini

Sekta binafsi nchini imekuwa na mchango mkubwa sana katika kuisaidia serikali kufanikisha malengo mbalimbali muhimu ya maendeleo.

Mfano mkubwa na makampuni ya mawasiliano nchini ambayo yamekuwa na mchango mkubwa sana wa kuboresha maisha ya mamilioni ya wananchi wa Tanzania. Makampuni hayo hujituma usiku na mchana kuhakikisha teknolojia zao inapatikana kwa wananchi, na kuwaunganisha wote lakini pia kuhakikisha wananchi waliokuwa wanakosa huduma za kifedha wanaweza kutumia huduma ya fedha kwenye simu.
Nchini Tanzania kuna jumla ya makampuni 8 ya simu, idadi ambayo ni kubwa sana miongoni mwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Unaweza ukadhani kuwa kwa wingi huo wa makampuni ya simu, kwamba huduma zitakuwa bora zaidi, si ndio! Basi unakosea, na kinyume chake ni sahihi.

Kupunguza wingi wa makampuni ya simu kutaruhusu uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo, jambo ambalo litaboresha utoaji huduma kwa wateja.

Kuunganisha kampuni mbili za simu kutatengeneza huduma bora kwa wateja. Mteja ambaye kwa sasa anapata huduma kutoka katika kampuni moja anaweza kupata huduma za kampuni zote mbili endapo zitaungana. Huduma hizo ni pamoja na huduma ya kifedha na upatikanaji wa mtandao (internet).
Hii inamaanisha kuwa mteja atapata huduma bora inayoendana na fedha anayotoa, ambayo ni upatikanaji wa mtandao wenye uwezo mkubwa kwa wakati. Hii itakuwa na faida kwa wateja wa pande zote mbili.

Licha ya kuwa sekta binafsi tayari imechangia kwa kiwango kikubwa katika maendeleo ya nchi, lakini bado kuna mengine mengi yanayoweza kufanyika kuinua mchango huo zaidi.

Tuimarishe soko la mitandao ya simu nchini ili kuhakikisha kuwa inasaidia nchi kusonga mbele kwa kasi kubwa iwezekanavyo.

Mwandishi wa Makala hii amejitambulisha kama mfanyabishara katika sekta ya mawasiliano nchini.

Send this to a friend