Kuungana kwa Tigo & Zantel kutakavyoboresha uchumi na sekta ya mawasiliano nchini Tanzania

0
15

Katika toleo maalumu la hivi karibuni jarida maarufu la Forbes Africa limeichambua sekta ya mawasilano ya simu nchini Tanzania kwa kuangalia ni kwa namna gani imeweza kulinufaisha taifa.

Tanzania inatarajia kufikia lengo la kuwa nchi ya uchumi wakati, uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025, na haipingiki kuwa sekta ya mawasiliano imekuwa na mchango mkubwa sana katika kufanikisha hilo.

Sekta hii imeleta mapinduzi katika maisha ya Watanzania wengi kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano na matumizi ya huduma ya fedha kwa njia ya simu.

Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) za mwezi Disemba 2018, jumla Watanzania milioni 43.5 wanatumia mitandao mbalimbali ya simu.

Pia kati ya mwaka 2009 hadi 2017 idadi ya Watanzania wanaotumia huduma rasmi za kuweka, kutuma na kupokea fedha imeongezeka kutokana na kukua kwa huduma hizo kupitia simu za mkononi.

Hii ni hatua nzuri kwani kwa kuangalia taarifa ya Tanzania National Financial Inclusion Framework 2018-2022 tunaona kuwa asilimia 55 ya Watanzania hawakuwa katika mfumo rasmi wa kutuma, kupokea na kuhifadhi fedha muongo mmoja uliopita.

Ili kuhakikisha kuwa sekta hii ya mawasiliano inaendelea kukua na kuboresha maisha ya wananchi, ni lazima mazingira rafiki kwa ukuaji wa sekta hii yatengenezewe.

Kwa hali iliyo sasa, kuna jumla ya watoa huduma nane wa mawasiliano ya simu za mkononi ambao wanashinda katika soko la Tanzania. Uimarishaji wa soko unashauriwa kuwa ndio njia pekee ya kuelekea mbele.

Katika toleo hilo la jarida la Forbes Africa, kuna mahojiano yaliyofanywa na Wakurugenzi Watendaji wa Makampuni yaTigo na Zantel, makampuni mawili ya mawasiliano nchini ambayo yemeeleza nia ya kuunganisha utoaji huduma (merger) kwa kuwa kampuni moja.

Katika mahojiano hayo, viongozi hao wamenukuliwa wakisemakuwa kuungana huko kutatengeneza mazingira ambayo yatawezesha kukua zaidi kwa sekta hiyo, huku wakitoa huduma bora kwa wateja wao.

Ni rai yetu kwa kila mpenda maendeleo ya Tanzania na sekta ya mawasiliano kuunga mkono nia hiyo njema ya kampuni hizi mbili ili kutengeneza soko imara na lenye ubora katika sekta ya mawasiliano litakalokuwa na tija na manufaa maradufu kwa wote.

Send this to a friend