Kwanini familia ya Rais aliyepinduliwa nchini Gabon inapigwa vita?

0
24

Familia ya Bongo imekuwa maarufu katika siasa za Gabon kwa zaidi ya miongo mitano. Omar Bongo alikuwa Rais wa muda mrefu wa Gabon kutoka mwaka 1967 hadi alipofariki mwaka 2009, na nafasi yake ilichukuliwa na mwanaye, Ali Bongo.

Familia ya Bongo imekuwa ikikosolewa vikali hasa kutokana na utajiri mkubwa walionao nchini humo. Uchunguzi wa polisi nchini Ufaransa uliofanywa mwaka 2007 uligundua kwamba familia ya Bongo ilikuwa ikimiliki mali 39 nchini Ufaransa, akaunti 70 za benki, na magari ya kifahari tisa yenye thamani ya jumla ya euro milioni 1.5 [TZS bilioni 4].

Kila ushindi wa uchaguzi anaopata Ali Bongo umekuwa ukikumbwa na mvutano mkubwa, mara nyingine ukisababisha maandamano makubwa yenye ghasia kote nchini. Uchaguzi wa hivi karibuni umepingwa vikali na upinzani kwa tuhuma za ulaghai ambao timu ya Bongo imekataa madai hayo.

Vivyo hivyo, mwaka 2016 baada ya Bongo kutangazwa mshindi wa uchaguzi, mpinzani wake mkuu alisema uamuzi wa mahakama ya katiba ya nchi kuthibitisha matokeo yaliyopingwa ulikuwa na upendeleo. Jaribio lingine la mapinduzi dhidi ya Bongo lilishindwa mwaka 2019.

Mapinduzi ya Gabon yamekosolewa sana na mataifa mengine ya Kiafrika na Magharibi. Umoja wa Afrika, unaojumuisha nchi wanachama 55, ulifanya mkutano wa dharura siku ya Jumatano, na rais wa tume alilaani mapinduzi hayo.

Kuchukua madaraka ni “uvunjaji wa wazi wa vyombo vya kisheria na kisiasa vya Umoja wa Afrika,” alisema Rais wa tume hiyo, Moussa Faki Mahamat katika taarifa huku akilitaka jeshi la Gabon kuhakikisha usalama wa Ali Bongo na kurejea kwenye utaratibu wa kikatiba wa kidemokrasia.

Send this to a friend