Kwanini watu huweka ‘airplane mode’ wakiwa ndani ya ndege?

0
54

Kuna sababu kadhaa kwa nini unashauriwa kuwweka ‘airplane mode’ kwenye simu yako wakati ukiwa ndani ya ndege.

Kwanza ni usalama wa ndege
Kuna wasiwasi kwamba ishara za mawasiliano kutoka kwa simu zinaweza kuingiliana na vifaa vya elektroniki vya ndege, kusababisha usumbufu na kuhatarisha usalama wa ndege. Hii haimaanishi kwamba simu yako inaweza kusababisha ajali, lakini ni hatua ya tahadhari kuzuia hali yoyote isiyotarajiwa inayoweza kusababisha hatari.

Vifaa vya kielektroniki vinavyotumiwa na abiria, kama vile simu za mkononi, tableti, na kompyuta, hutumia teknolojia ya ‘wireless’ ili kutumia huduma kama Wi-Fi, Bluetooth, na mitandao ya simu. Teknolojia hii inazalisha taarifa (signal) za redio ambazo zinaweza kuingiliana na vifaa vya mawasiliano ya ndege, ambayo inaweza kusababisha usumbufu wa mawasiliano ya radio kati ya ndege na mnara wa uwanja wa ndege au kati ya ndege na ndege nyingine.

Orodha 10 ya nchi za Afrika zenye mamilionea wa dola wengi zaidi

Ingawa hatari ya kuingilia mifumo ya ndege na vifaa vya elektroniki vya abiria ni ndogo, inaweza kutokea. Kwa mfano, katika miaka ya hivi karibuni, kulikuwa na ripoti za vifaa vya elektroniki vinavyoweza kuingiliana na mifumo ya ndege na kuathiri kazi ya vifaa vya ndege, kama vile ripoti za simu za mkononi zinazoingiliana na mifumo ya ndege, lakini ripoti hizi zilikuwa chache sana.

Kuwapa wafanyakazi wa ndege nafasi
Wafanyakazi wa ndege wanahitaji nafasi ya kufanya kazi yao kwa ufanisi na kuwahudumia abiria wote pamoja na kutoa maelekezo muhimu wakati wa safari. Simu zinazotoa miito na ujumbe za maandishi zinaweza kuwafanya wafanyakazi wa ndege washindwe kufanya kazi yao vizuri na kuhatarisha usalama wa ndege.

Send this to a friend