Kwanini watu wengi wanapata maumivu ya kichwa mara kwa mara?

0
67

Siku hizi watu wengi hususani ni vijana, wanalalamika kupata maumivu ya kichwa, uchovu wa macho, kuona giza, kuhisi uchovu na mengineyo mengi.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa matumizi ya mara kwa mara ya simu yako ya mkononi, kompyuta na televisheni au kwa ujumla tunasema skrini zote unazotumia ikawa sababu ya matatizo hayo.

Watu wanaotazama skrini na vifaa kila mara wanaweza kupata mkazo wa macho na mengine mengi kulingana na utafiti wa hivi majuzi uliochapishwa katika Jarida la Sayansi ya Matibabu la Cureus.

Ni nini hasa husababisha matatizo ya macho yanayotokana na vifaa vya dijitali?

Kwa mujibu wa wataalamu, vifaa vya kidijitali kama vile kompyuta na simu janja hutoa mwanga wa samawati (blue). Na mwanga wa bluu unapoingia kwenye jicho, hutawanyika kabla ya kufikia retina, na kusababisha macho yetu kutumia nguvu kubwa ili kujaribu kuzingatia na kuchakata mwanga unaotoka kwenye vifaa vyetu.

Dalili za mkazo wa macho unaotokana na matumizi ya vifaa vya elektroniki zinaweza kujumuisha uoni hafifu, macho kuchoka, macho kuuma, maumivu ya kichwa, na macho kuwa makavu.

Jinsi ya kuepuka kuishiwa pesa mwezi Januari

“Madhara haya ni matokeo ya misuli katika macho yetu kufanya kazi kupita kiasi kwa kuangalia zaidi skrini kwa ukaribu. Tunapotumia vifaa vya kidijitali, hatupepesi sana macho, kwa hivyo macho yetu hayapati kiwango sahihi cha ulainishaji hivyo kusababisha macho kuwa makavu na kuwasha, mtaalamu Danny Mathew kutoka Marekani anaeleza.

Watu wanaweza kufanya nini ili kupunguza hatari za matatizo ya macho yanayosababishwa na vifaa vya kidijitali?

Kuweka skrini ya kompyuta au simu mbali na wewe ni njia rahisi ya kusaidia kupunguza msongo wa macho. Pia, kurekebisha mwanga wa kifaa chako ni hatua nyingine rahisi inayoweza kusaidia kupunguza mng’aro na mkazo wa macho

Ni mabadiliko gani ya kila siku yanayoweza kupunguza mkazo wa macho unaotokana na matumizi ya vifaa vya kidijitali?

Wataalam wanasema kila wakati unapojikuta unatumia muda mrefu kutazama kifaa cha kidijitali, inuka, tembea, nyoosha mwili wako au angalia nje ya dirisha ili kuyapa mapumziko macho yako.

Send this to a friend