Kwanza Online TV kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa TCRA

0
41

Kituo cha Televisheni Mtandaoni (Kwanza Online TV) imesema kuwa itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wa kukifungia kutotoa huduma kwa miezi 11, kwa madai kuwa haki yao ya kusikilizwa haikuzingatiwa.

Uamuzi huo wa Kwanza Online TV umekuja siku chache baada ya Kamati ya Maudhui ya TCRA kukifungia kituo hicho kwa maelezo kuwa kilichapisha habari inayokiuka Kanuni za Maudhui ya Kielektroniki na Posta za Mwaka 2018.

Kiongozi wa kamati hiyo Joseph Mapunda alisema kuwa taarifa ya Ubalozi wa Marekani kuhusu hali ya corona nchini Tanzania iliyochapishwa na kituo hicho ni ya uongo na ililenga kusababisha taharuki na pia kuathiri biashara ya utalii na uchumi wa nchi.

Kwa upande wao, Kwanza Online TV wamesema kuwa hawakupewa muda wa kutosha kujieleza, hivyo adhabu hiyo imekiuka taratibu za msingi.

Hii ni mara ya pili kwa kituo hicho kufungiwa ambapo mara ya kwanza kilifungiwa kwa muda wa miezi sita baada ya kukutwa na hatia ya kutoa taarifa inayohusu Dkt. Gwajima kupata ajali bila kutaja jina la kwanza jambo lililoelezwa kufanywa kwa makusudi kuikuza habari

Send this to a friend