Lady JayDee adaiwa kuhamasisha uvutaji bangi

0
53

Wimbo unaokwenda kwa jina la One Time wa mwanamuziki Judith Wambura, maarufu, Lady JayDee upo kwenye hati hati ya kufungiwa kwa madai ya kuchochea uvutaji bangi.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema kuwa limepokea malalamiko kutoka kwa wadau wa muziki na linafanyia kazi maoni yaliyowasilishwa kuhusu wimbo wa nguli huyo wa bongo fleva.

“Tumeliona hilo na suala hili lipo kwenye position [nafasi] ya kufanyiwa kazi, baada ya kuifuatilia. Kwa hiyo, niishie kusema tu kwamba, tunaendelea kulishughulikia jambo hili baada ya kufanya uchunguzi,” amesema Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza.

Lady JayDee ambaye amekuwa kwenye ulingo wa bongo fleva kwa miaka 20 aliuachia wimbo huo Septemba 14 mwaka huu.

Send this to a friend