LATRA: Hakuna mwananchi atakayeshindwa kulipa ongezeko la nauli

0
64

Baraza la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) limesema kuna sababu mbalimbali za kuongezeka kwa nauli zikiwemo uendeshaji wa usafiri huo na kupanda kwa bei ya mafuta.

Akizungumza hapo jana Katibu Mtendaji wa LATRA CCC, Leo Ngowi amesema ongezeko hilo ni makubaliano kati yao na Serikali kupitia kikao walichoshirikishwa cha majadiliano kilichofanyika mwezi uliopita jiini Dar es Salaam.

Petroli yashuka, dizeli yapanda kuanzia Januari 4, 2023

Ngowi amesema katika kikao hicho cha maoni, wadau walipendekeza ongezeko kubwa la nauli ambapo walishauri iongezwe ikilinganishwa na hali halisi ya maisha na kwamba wanaamini ongezeko hilo la TZS 100 hakuna mwananchi  atakayeshindwa kuilipa.

“Tunaishukuru Serikali kwa kukubali maoni yetu na hivi sasa nauli ya mwendokasi imeongezeka kwa TZS 100,” amesema Ngowi.

Send this to a friend