LATRA: Nauli hazitashuka

0
37

Baada ya bei ya mafuta ya petroli, dizeli kushuka, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imesema hawana mpango wa kushusha nauli kwa sababu uendeshwaji wa vyombo vya usafiri hautegemei gharama za mafuta pekee.

Akizungumza na gazeti la Tanzania Daima, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe amesema gharama za mafuta zinategemewa kwa asilimia 38 tu, na asilimia 62 ni gharama nyingine.

“Nauli imeongezeka siyo kwa sababu ya kupanda kwa gharama za mafuta. Nauli zilizopo tumeangalia vitu vingi, tumeangalia pia wastani wa bei za mafuta kwa mwaka mzima, kwa hiyo hata kama mafuta yatashuka, haitaathiri nauli tulizoziweka,” amesema.

Hata hivyo, amesema watakaa na kulijadili suala hilo endapo kutakuwa na mabadiliko makubwa ya kushuka kwa bei ya mafuta.

Send this to a friend