LATRA yapokea mapendekezo ya nauli mpya za Mwendokasi

2
59

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imewataka wadau kutoa maoni yao baada ya kupokea maombi ya mapendekezo ya viwango vipya vya nauli za mabasi yaendao haraka mkoani Dar es Salaam (BRT).

Ameyasema hayo Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe baada ya kupokea taarifa ya maombi kutoka kwa kampuni ya wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) juu ya mapendekezo ya viwango vipya vya nauli.

Aidha, amewataka wadau na wananchi wote kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika Mei 26 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam saa 3 asubuhi kutoa maoni yao juu ya mapendekezo hayo.

Ameongeza, kwa mujibu wa kifungu namba 21 cha Sheria na 413, mamlaka inapaswa kukusanya maoni ya wadau kabla ya kufikiwa uamuzi kuhusu viwango vipya vya nauli vinavyopendekezwa.

Send this to a friend