Libya: Benki Kuu yasitisha huduma baada ya Mkuu wa Idara ya Habari kutekwa

0
38

Benki Kuu ya Libya imesitisha shughuli zote na kutangaza kutoendelea hadi Mkurugenzi wa Idara ya Teknolojia ya Habari wa benki hiyo, Musab Msallem aliyetekwa nyara siku ya Jumapili atakaporejeshwa.

Msallem alitekwa nyara akiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana ambapo pia tukio hilo limehusishwa na tishio la utekaji nyara wafanyakazi wengine wa benki hiyo.

Utekaji nyara umekuja wiki moja baada ya watu wenye silaha kuzingira benki na kulazimisha kujiuzulu kwa gavana wake, Seddik al-Kabir, ambaye amekuwa akikosolewa kutokana na usimamizi wake tangu ashike nyadhifa hiyo mwaka 2012.

Send this to a friend