Lindi: Watoto wa miaka 8 wachomwa sindano za kuzuia mimba

0
45

Baadhi ya wazazi wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi wamedaiwa kuwalazimisha watoto wao wa kike kuchomwa sindano za kuzuia kupata ujauzito kitendo kinachowaweka hatarini kukumbwa na tatizo la utasa hapo baadaye.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma wakati wa mdahalo wa kujadili kero zinazowakabili vijana wakiwemo wanaoishi na Virusi vya Ukimwi katika maadhimisho ya Wiki ya Ukimwi Duniani.

Ameongeza kuwa katika Wilaya anayoiongoza  amebaini watoto wa kike walio na umri kuanzia miaka minane hadi 13 wanachomwa sindano za kuzuia wasipate ujauzito huku wazazi wakidaiwa kuweka msisitizo kwa watoto hao kuchomwa sindano hizo jambo linalochangia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na ugumba.

Mambo 7 ambayo wanawake hawawezi kuvumilia kwenye mahusiano

Ngoma ameeleza kuwa watoto wa kike hivi sasa hawahitaji matumizi ya kondomu kutokana na matumizi ya sindano ya kuzuia kupata ujauzito, huku baadhi ya shule zikiwamo za msingi ndani ya Wilaya hiyo kuwa na idadi ndogo ya wanafunzi kutokana na kushiriki zaidi mapenzi  kuliko masomo.

Send this to a friend