Lissu aeleza anapopata uhalali wa kugombea urais licha ya kuvuliwa ubunge

0
39

Wakili Tundu Lissu ambaye ametangaza nia ya kugombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema kuwa anafahamu kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakihoji kama ana uhalali/sifa za kikatiba na kisheria za kugombea nafasi hiyo ya juu nchini.

Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii kutoka nchini Ubelgiji, Lissu amesema hoja hiyo imeibuliwa kutokana na kuvuliwa nafasi yake ya ubunge Juni 2019.

“Mtu anayekosa sifa za kugombea urais (au ubunge) ni yule tu ambaye amepatikana na hatia ya kukiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na chombo pekee kilichoanzishwa kwa mujibu wa sheria hiyo, yaani Baraza la Maadili,” amesema Lissu.

Ameongeza kuwa katika utumishi wake kama kiongozi wa umma, mimi sijawahi kutuhumiwa, kushtakiwa, kuitwa kwenye shauri, kutolewa ushahidi wowote dhidi au kwa niaba yangu, na kuhukumiwa na Baraza la Maadili kwa kosa lolote lile chini ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Hivyo, amesema kufutiwa kwake ubunge hakujamuondolea sifa za kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au nafasi nyingine yoyote ya uongozi, kwa sababu uongozi wa bunge hauhusiani Baraza la Maadili.

Send this to a friend