Lissu akamatwa kwa kufanya mikusanyiko isivyo halali

0
39

Jeshi la Polisi limethibitisha kumshikilia Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu pamoja na wenzake watatu wa chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, Lissu ameshikiliwa kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tuhuma za kufanya mikusanyiko isivyohalali na kuwazuia askari Polisi kutekeleza majukumu yao.

Aidha, polisi wamesema baada ya mahojiano hayo na ukamilishwaji wa taratibu nyingine, hatua nyingine za kisheria zitafuata.

Wengine wanaoshikiliwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Susan Kiwanga, Katibu BAWACHA Taifa, Catherine Ruge na Twaha Mwaipaya.

Send this to a friend