Lissu: CHADEMA kuna mtafaruku na fedha chafu

0
47

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema kuna fedha nyingi ndani ya chama hicho ambazo hazijulikani zinatoka wapi, fedha zilizoibuka hivi karibuni wakati nchi ikielekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na uchaguzi ndani ya chama.

Ameyasema hayo wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara mkoani Iringa ambapo ameeleza kuwepo kwa mtafaruku mkubwa ndani ya chama hicho kutokana na fedha hizo ambazo si za chama, alizoeleza kuwa zinakiweka chama kwenye hatari.

“Kuna mtafaruku mkubwa sana wa uchaguzi ndani ya chama chetu. Kuna pesa nyingi ajabu kwenye uchaguzi huu, hela ambayo tukisema tufanye mikutano, tutafute vyombo vya matangazo huwa haipo. Leo kwenye uchaguzi kuna hela ya ajabu, nyinyi mnafikiri hii hela ni ya wapi? Mnafikiri hii hela itatuacha salama? Ukitaka kujua kuwa hatuko salama, fuatilia mitandaoni […] Hizo pesa sio za CHADEMA kwa sababu sisi huwa hatuna hela zozote,” amesema Lissu.

Tundu Lissu apingwa kwa madai ya kauli yake ya kibaguzi

Ameongeza kuwa “niliambiwa nisije kuzungumza kwenye mkutano huu. Niliambiwa nisubiri uchaguzi upite ndio nije […] nikasema hapana nitakuja nije nizungumze hadharani, nije niwape za usoni. Nawaombeni wanachama wa Iringa, muwe macho na hizi pesa zitatuangamiza tusipoangalia, na sio Iringa peke yake, kila mahali.

Hata hivyo, Lissu amewasihi wananchi kuchagua viongozi ambao ni waaminifu ili kuleta manufaa kwenye chama hicho.

Send this to a friend