Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi

0
115

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, Katibu Mkuu, John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (Sugu) wamekamatwa na Polisi mkoani Mbeya katika ofisi za CHADEMA kanda ya Nyasa leo.

Viongozi hao wamewasili leo mkoani humo ili kuungana na vijana wa chama hicho kupitia Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) waliokuwa wameandaa maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani yaliyopangwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.

Mapema leo Jeshi la Polisi lilipiga marufuku maandamano na mikusanyiko yaliyopangwa na viongozi wa chama hicho kwa mwamvuli wa kuadhimisha Siku ya Vijana kutokana na kauli zao ambazo zimeashiria uvunjifu wa amani.

 

 

 

Send this to a friend