Lowassa alazwa Afrika Kusini kwa matibabu

0
43

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na wanafamilia jijini Johannesburg Waziri Mkuu amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Rais na kusema anafuatilia hali ya Lowassa kwa ukaribu na anamwombea afya njema.

Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao.

Naye mtoto wa Lowassa na Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.

Send this to a friend